Mwimbaji wa Injili kutoka Tanzania Sifa John anatarajia kufanya Tamasha kubwa la uimbaji ambapo atazindua album yake USILILIE MOYONI na huduma yake SIFA EBENEZER FOUNDATION siku ya tarehe 29/4/2012 viwanja vya Biafra.
Akiongea na Strictly Gospel dada Sifa anaielezea SIFA EBENEZER FOUNDATION โnina mzigo wa kusaidia watoto, vijana na mabinti wasiojiweza, kuwasaidia waondoke kwenye mazingira magumu, kutoshawishika kufanya vitendo viovu, kufundishwa ujuzi mbalimbali, kuinua vipaji vyao pia na kupatiwa semina mbali mbali za kirohoโ.
โMgeni rasmi atakuwa Emmanuel Nchimbi, pia ninawakaribisha wadau wote kuhudhuria siku hiyo waimbaji wengi wataimba na kumtukuza Bwanaโ alimalizia kusema dada Sifa.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na dada Sifa kwa email,ย sifajohn@ymail.com
Filed under: SINGERS
