Sikiliza wimbo wa Kamata Pindo….
Uzinduzi wa album mpya ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rose Muhando inayoitwa “KAMATA PINDO LA YESU”unatarajiwa kufanyika August 03 2014 katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE, kuanzia saa 7 kamili mchana jijini Dar es salaam Tanzania, ambapo waimbaji wote waalikwa wataimba LIVE, ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe Mwimbaji anayelitukuza jina la Mungu Tanzania ROSE MUHANDO.
Album hiyo yenye mpya kama FACEBOOK, NA KAMATA PINDO LA YESU, na nyinginezo zitakuwa katika video na audio.
Video imetengenezwa na kampuni ya MSAMA VIDEO PRODUCTION, ambayo ni kampuni mpya dada ya MSAMA PROMOTIONS.
Mkurugenzi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ndugu ALEX MSAMA ambaye ndiyo waandaji wa tamasha hilo, amesema kuwa maadalizi ya uzinduzi huo mpaka sasa yapo tayari na wadau wa muziki wa injili wakae tayari kumtukuza Bwana kwa siku hiyo.
Filed under: SINGERS
